SEHEMU YA 4
ILIPOISHIA.....
"Nakwenda kumuomba akinipa sawa akininyima pia sawa,vyovyote itakavyokuwa"Aliwaza Subi akimsogelea yule binti mlaji wa chipsi.Anamfikia lakini mdomo unakuwa mzito kutamka anabaki akimtizama tu.Alimwangalia kwa jicho la huruma,jicho la kuomba lakini binti hakuweza kutambua hilo aliendelea kula chipsi yake Taratibu kwa pozi kama anajilazimisha pasi na kujua anamtesa mtoto Subi.
_____SONGA NAYO_________
Mara simu ya yule Dada inaanza kuita,anatazama kioo Cha simu yake ya Bei Kali,"waooo my love"haraka anaipokea na kuiweka sikioni.
"Hello Darling"anaongea kwa sauti laini huku akiinyanyuka kidogo na kusogea pembeni.Bila kugundua anadondosha pochi yake,simu imempa pumbazo hakumbuki Tena Kama yu safarini,ahofii Tena usalama wa mizigo yake.Akili yote imetekwa na simu ya mpenzi wake.
Wakati huo Subi bado anazitolea macho chipsi za huyo dada,wala hakuwa na habari na pochi iliyodondoshwa na Dada huyo.Macho na akili yake yote ilikuwa juu ya chakula, Moyoni akaisikia sauti ikimsukuma achukue chipsi hizo,huku sauti nyingine ikimzuia kufanya hivyo.Ilikuwa ni Kama mpambano wa sauti hizo mbili,akawa akinyoosha mkono kidogo anasita anaurudisha nyuma kisha anaunyoosha tena kwenye chipsi halafu anaurudisha.Njaa haina adabu hatimae sauti ya kumsukuma achukue inashinda mpambano.Anachukua chipsi nakuanza kula huku akisindikizia na soda.
"Pumbavu Wewe,Nani kakuruhusu uchukue chipsi zangu?"Sauti kali inapenya masikioni mwa Subi,anashtuka na kumtazama muongeaji.Macho yake yanagongana ana kwa ana na macho ya Dada huyo.Subi anaogopa Sana lakini haachi kula anaendelea kula huku akimtizama Dada huyo kwa uoga.
"Fyuuuuu,chokoraa mkubwa Wewe unaendelea kula,unajua gharama ya hivyo vyakula?,yaani unakunywa mpaka soda yangu!"Aliongea Dada yule kwa ukali akachukua zile chipsi akammwagia Subi mwilini hakuishia hapo akachukua soda iliyobaki kwenye kopo nayo akammwagia kichwani.Akamalizia kwa kumpiga mateke mawili huku akichukua begi lake na kuanza kupiga hatua kuondoka.
Anapiga hatua mbili ya tatu anakumbuka kitu,anajipapasa kwenye mifuko ya suruali ya Jeans aliyovaa,haoni kitu anarudi mpaka eneo alipokuwa amekaa na Subi.Anavua begi lake na kufungua zipu,anaanza kupekuapekua ndani ya begi hilo.Anatoa nguo,makaratasi,vipodozi na kila kilichokuwemo Lakini bado haoni anachokitafuta.Anakung'uta begi kwa nguvu anaishia kudondoka mende na vumbivumbi tu.
Pochi!,naam ni pochi ndio iliyokuwa ikitafutwa na Dada huyo aliyeonekana kuchanganyikiwa.Pamoja na kwamba pochi hiyo haikuwa na dhahabu wala Tanzanite, lakini pochi hiyo ndio iliyobeba Pesa,tiketi,kadi za Benki,Vitambulisho na nyaraka zote muhimu.
"Pochi imeenda wapi?,au imeibiwa?.Na imeibiwa Vipi wakati nilikuwa nayo hapahapa?.Au nimeidondosha njiani? Lakini mbona nakumbuka nilikuwa nayo kwenye begi na niliitoa Mara Baada ya simu kuita?!."Anajiuliza maswali mengi kichwani maswali ambayo alijijibu mwenyewe.
"Hapana,Itakuwa huyu Mtoto kanifichia.Ndio, lazima atakuwa ni yeye maana ndiye aliyedokoa hata chipsi,yes ni huyuhuyu tu"Anawaza huku akimtizama Subi kwa jicho Kali,hasira zinampanda.
Anamsogelea Subi,anamshika masikio yake na kuanza kuyavuta juu juu mpaka akasimama wima.
"Pochi yangu iko wapi?"Aliongea akiwa kamshika gauni yake akimtikisa huku na kule.
"Mi.mi...sijui"Subi alijibu huku akilia masikini,Ni kweli hakufahamu lolote kuhusu pochi ya Dada huyo.Isitoshe hata neno pochi kwa Mtoto huyo ulikuwa Ni msamiati,msamiati uliohitaji atumie kamusi ama aonyeshwe picha ndipo angebaini maana ya neno Hilo.
"Hujui wakati Ni wewe ndiye umeificha,toa pochi yangu Mtoto takuumiza"Sasa alimshika mashavu nakuyavuta kwa nguvu,watu waliokuwa jirani hawakushangaa kwani kwa muonekano tu haswa mavazi walishajiaminisha Mtoto huyo Ni chokoraa,kundi ambalo ni tishio kwa kukwapua vitu vidogovidogo maeneo yenye mikusanyiko ya watu.Na hali hiyo ilitokana na kundi hilo kukosa mahitaji stahiki na kuishia kwenye vitendo vya uhalifu.
Wengi wao walikuwa ni watoto yatima ambao walipoteza wazazi wao angali wakiwa wadogo,wengine walitoroka majumbani mwao kutokana na sababu mbalimbali kama vile mateso, vilevile wapo pia waliotelekezwa na wazazi au Ndugu zao wa karibu na kuamua kuingia mitaani kuanza Maisha mapya.
"Lete pochi yangu paaah"Anaongea tena huku akirusha Kofi moja zito shavuni mwa Subi,sekunde tatu Kofi la pili linatua kwenye shavu la kulia.Kofi hilo linampeleka Subi chini bila kutarajia.Anaachia ukelele "Mamaaaa"Kisha anatulia kimya.Tayari watu walishajaa kushuhudia tukio hilo,wakisukumana na kukanyagana mithili ya watu wanaogombania chakula.
****
"Vipi shosti leo huendi kunywa uji?"
Ilikuwa ni sauti ya msichana mmoja aitwaye Aisha,Ni msichana ambae anasifika Sana kwa uongeaji shuleni hapo, Nguvuni shule ya sekondari,yenye wanafunzi mchanganyiko wavulana na wasichana,kidato Cha Kwanza mpaka Cha nne.
Uongeaji wake Aisha unamfanya ajipatie marafiki wengi kwa muda mfupi tu.Na Sasa alimpata rafiki mpya aitwaye Queen,ni msichana mgeni aliyehamia shuleni hapo,mwezi mmoja tu uliopita.Aisha alitokea kumchangamkia Sana msichana huyo mpole na mrembo Kama jina lake lilivyo.Iliwachukua wiki mbili tu wakawa marafiki wakubwa,wakila chakula pamoja,wakilala bweni moja,wakikaa meza moja darasani hata kubadilishana Siri zao.
"Sijisikii nenda tu"alijibu Queen huku akifungua daftari yake ya rafu na kuanza kuchorachora.
"Twende shosti au unataka chai?,Leo mama Juma hajaja"AnaongeaAisha akimsihi mwenzake waende kunywa uji kwenye ukumbi wa kulia chakula walipopenda kupaita"Dinning Hall".Mara anamuona mwalimu wao akiingia humo darasani nakuwafuata moja kwa moja mezani walipokuwa wameketi.
"Aisha, mbona mwenzako kajiinamia?"Ni sauti ya mwalimu wao wa Nidhamu ambaye pia huwafundisha somo la Kemia.
"Anaumwa sijui atakuwa anaumwa"Anajibu Aisha kwa woga,pamoja na uongeaji wake wote lakini kwa mwalimu huyo alikuwa anapooza na kuwa mdogo Kama punje ya haradali.Hii ilitokana na ukali wa mwalimu huyo mwenye sura Mbaya ya kutisha.
"Ndio jibu gani hilo?,Amekunywa chai?"Anauliza huyo mwalimu almaarufu Kama Zinja Makasi,jina la utani alilopewa na wanafunzi wa kiume hapo shuleni kulingana na umbo pamoja na tabia yake.
"Hapana"Aisha anajibu.
"Kwanini?"Mwalimu Zinja Makasi anauliza tena kwa sauti yake nzito.
"Mama Juma hajaja Leo"Anajibu.
Mama Juma ni mmoja wa wauzaji wa chai kwenye kantini ya wanafunzi,muuzaji ambae hupendwa zaidi na wateja wake kutokana na huduma zake Bora na kuzingatia usafi.
"Nifateni"Anaamrisha Mwalimu Zinja Makasi,Kisha anageuka na kuelekea nje ya darasa hilo la kidato cha pili B.
Wananyanyuka nakuongozana na Mwalimu wao,Safari yao inaishia ndani ya chumba Cha kantini ya walimu.Harufu nzuri ya vyakula ambavyo ni muda mrefu hawajaihisi inaburudisha pua zao.
"Madam huyu binti Ni mgonjwa wapatie chai ya maziwa, chapati mbili na yai mojamoja"anatoa amri mwalimu Kisha anawageukia wanafunzi wake"kuleni haraka muwahi darasani."
Baada ya hapo anatoka kantini akiwaacha wanafunzi wake,Aisha alifurahi sana ni muda mrefu hakupata chai ya maziwa,mayai ndio kabisa alishasahau hata ladha yake.
Hali ilikuwa tofauti upande wa Queen,uso wake ulionyesha wazi hakuwa na furaha.Muda wote alikuwa kimya,mdomo aliuvuta lile tabasamu lake lililozoeleka kuupamba uso sambamba na vishimo vidogo kwenye mashavu yake havikuonekana tena.
"Badala ufurahi tumepewa ofa, wee unavuta mdomo"Aliongea Aisha akimshangaa rafiki yake,wakati huohuo mpishi anawatengea chai na vyote alivyoambiwa.Aisha anachangamka kula mpaka anamaliza ndipo anashtuka kumtizama mwenzake.
"Heee mbona huli shosti?"Anauliza kwa mshangao lakini rafiki yake hajibu na zaidi amejiinamia kwenye meza.
"Umekuaje Wewe?,au unaumwa Sana?"Anauliza Tena Aisha huku akijaribu kumuinua kichwa,anafanikiwa nakukutana na Hali ambayo hakuidhania meza yote alipolaza kichwa Queen imeenea machozi.Anashtuka zaidi kugundua rafiki yake huyo amepoteza fahamu."Mmmh"Anaguna Aisha,anatoka mbio mpaka ofisini kwa Matroni.
Queen kakumbwa na nini?,kulia tu mpaka kupoteza fahamu.Vipi hatma ya Subi?
Usikose sehemu ijayo.. ITAENDELEA