Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Test link

SIMULIZI: CHOZI LANGU LITAFUTWA LINI? Sehemu ya 2

SEHEMU YA 2


ILIPOISHIA.....
Binti huyo alitembea kwa kuchechemea huku akitizama huku na kule,aliendelea kutembea taratibu huku mara kadhaa akiinama na kushikilia magoti, muda ulivyozidi kwenda ndivyo alivyozidi kuchoka miguu yake ilianza kuuma alitamani kupumzika lakini alihofia usalama wake.Binti akiwa amechoka sana alianza kusikia muungurumo mkubwa ukija nyuma yake aliogopa sana nakutaka kujificha,akageuka aanze kurudi vichakani lakini kabla hajafanya chochote alimulikwa na mwanga mkali usoni.Mwanga huo ukamfanya apoteze uelekeo akipepesuka kidogo Kisha akachuchumaa chini huku akifunika uso wake kwa viganja vya mkono.
______SONGA NAYO________
Mwanga unapungua,Anasimama wima kisha anatoa mikono usoni na hapo ndipo alipogundua kuwa ile ilikuwa ni gari,hakuwahi kupanda gari lakini alikuwa akiyaona baadhi yakifika kijijini kwao Itobela kubeba magunia ya mahindi.Alimshuhudia kijana mwenye umbo kubwa lililojazia vizuri akishuka kwenye gari,tuseme ni Lori.Kijana yule alijongea mpaka alipokuwa amesimama mtoto.
"Unafanya nini hapa usiku huu?"ilikuwa ni sauti nzito ya dereva, sauti iliyomfanya mtoto yule azidi kuogopa.
"Mama mama"alijibu binti huyo huku akisita kuendelea zaidi.
Dereva alitambua hofu ya binti huyo,akamwambia asiogope.Alimuuliza maswali wawili matatu na binti huyo alimweleza alikuwa akitaka kwenda mjini kwa mama yake kwani baba yake anataka kumuozesha,Dereva hakushangaa kwani alishasikia visa vingi vya mabinti wadogo kulazimishwa kuolewa,na wachache Sana huokoka kwa kutoroka nyumbani huku wengine wakichukua maamuzi magumu Kama kujitoa uhai.Alimuuliza mtoto yule kama anafahamu anapoishi mama yake binti akaitikia kwa ishara kuonyesha ndio, Basi dereva akaridhika na majibu hayo hakutaka kumuuliza zaidi.Alimuoneahuruma asingeweza kumuacha mahali pale usiku kama huo alimshika mkono na kuingia nae kwenye gari na safari ikaanza.

Ndani ya gari binti alikuwa akitabasamu Aliomba kimyakimya na Kushukuru Muumba wake kwa msaada huo,aliamini sasa ameepukana na kadhia iliyokuwa ikimuandama.Aliwafikiria mabinti wengine wenye rika Kama lake kijijini,aliwasikitikia sana akajiapiza lazima siku moja arudi kuwasaidia.
"Nasema lazima nitawaokoa,Ee Muumba nisaidie"Alijikuta Akiongea kwa sauti kubwa huku akijipigapiga ngumi kwenye kiganja chake Cha mkono wa kushoto.Sauti hiyo iliwashtua dereva na mwenzake,wote waliguna huku wakimtazama binti huyo ambae alionekana kugwaya.
"Unasema utawaokoa?,akina Nani?"Kijana mwenzake dereva alidodosa akitegemea kujibiwa chochote Lakini tofauti na matarajio yake binti hakujibu kitu.
"Weweee Si nakuuliza wewe husikii au?"Aliongea Tena yule kijana akiwa kakunja uso na kumkazia macho yule mtoto, hakuridhika akawa akimvutavuta shavu kwa nguvu.
"Hebu muache,wee Jamaa unapenda Sana kujua mambo yasiyokuhusu,hivi utaacha lini kupenda udaku?"Dereva aliingilia Kati na kumgombeza msaidizi wake baada ya kuona binti amekosa Amani na kuanza kutiririkwa na machozi.
"Hamna Cha udaku bosi,hivi unakumbuka tabia ya kubebabeba watu hovyohovyo njiani ilivyowahi kutucost?, ngoja nikusimulie Sasa"Aliongea msaidizi wa Dereva.
"Enheee ilikuwaje?"Dereva aliitikia kuruhusu msimuliaji aanze.

Anaanza kusimulia"Ilikuwa mwaka 2009 Kama sikosei,tulikuwa na Safari ndefu tuliendesha gari kwa mwendokasi na hatukutaka kulala njiani,baada ya kufika boda wenzetu walitushauri tulale Mana mbele Kuna msitu mkubwa ambao ni hatari."Anaweka kituo kidogo anafungua chupa yake ya maji anakunywa mafunda matatu Kisha anairudisha pembeni,wakati huohuo anageuka kumtizama binti aliyekuwa makini kumsikiliza.
Anaendelea"Basi tukajifanya wabishi kwa kuwa tu tulikuwa na mguu wa kuku(bastola) tukasema kipi kitatutisha?,tukaendelea na Safari mpaka msituni, tulikuwa watatu Mimi,Dereva na Jamaa mwingine.Tukiwa ndani ya msitu gari ikikanyaga mafuta kwa Mbali tukamuona mzee wa makamo akipunga mkono alionekana kuchoka Sana na mgongoni alikuwa kabeba begi,basi tulimuonea huruma tukampa lifti."
"Enhee ikawaje"Dereva akadakia.
"Dah kumpa lift ikawa majanga,yaani sitokuja kusahau,Mtu huyo baada ya kuingia kwenye gari alituambia yeye ni mfanyabiashara wa madini,huku Mara kadhaa akishika vizuri begi lake Kama vile anataka kufungua zipu,Mara aweke begi sikioni Kama anasikiliza kitu.Basi hatukumjali tukawa bize na stori zetu za wanawake, ghafla harufu Kali ya uozo ikaanza kusikika ikabidi tugeuke pembeni kutizama,haaaa,mtu yule kaoza"
"Wee,Acha zako kaoza,kaoza kivipi?"Dereva akadakia.
"Kaoza bosi kaoza mwili wote funza wanamtembea,Si machoni puani mwili woteee"anaongea msaidizi wa Dereva huku akionyesha kwa ishara.
"Sasa kwanini aoze?"Dereva aliuliza.
"Mi sijui Bosi,ila nahisi alikuwa kwa mganga na mule kwenye gari akakiuka masharti"Alijibu msimuliaji.
"Mkampeleka hospital?"Binti akavunja ukimya kwa kuuliza swali.
"Weeee Nani ampeleke hospital, Dereva aliitupa gari tukaruka mbio kila mtu kivyake,tulikuja kuzinduka tupo hospital"Anaongea huku wote wakiangua kicheko.
"Hamkuumia Lakini?"binti anauliza Tena.
"Mmoja wetu alikufa,Mimi niliumia hapa"anawaonyesha kovu kubwa maeneo ya begani.
"Hizo ni changamoto tu za kazi,uchawi,majambazi ni kuomba Mungu tu ulinzi wa.."kabla Dereva hajamaliza kuongea Gari inazima.
"Dah nini Tena"Msaidizi wa Dereva anamtizama binti kwa jicho la hasira"Bosi nimekwambia huyu dogo hafai kuwa humu analeta mikosi hii"
"Wacha ujinga wewe,shida ni maji"Anajibu Dereva ambae tayari ameshuka na kwenda kukagua kwa mbele ya gari.
"Tulisahau akiba dah,tukatafute Basi huko kwenye vijiji"Anatoa wazo.
"Baki humu,sisi tukatafute maji"Dereva alimwambia binti 
"Hapana naogopa twende tu wote"Binti alijibu huku akishuka kwenye gari.Pamoja na kuwa amechoka Sana Lakini hakukubali kubaki peke yake,bado alijawa hofu ukiongeza na simulizi aliyoisikia muda mfupi alihisi kuchanganyikiwa kabisa.Waliongozana wote watatu wakitafuta Kijiji chochote hapo karibu waweze kupata maji,kwa mbali juu ya kilima waliona Moto ukiwaka.Hali hiyo iliashiria eneo Hilo Kuna watu wanaishi japokuwa kulikuwa ni porini.

Walipita vichakani kwenye nyasi fupifupi kufuata mwelekeo wa Moto huo,taratibu kwa msaada wa mwanga wa kurunzi wanafanikiwa kufika, kulikuwa na nyumba moja ndogo Sana ya nyasi aina ya msonge, pembeni kulikuwa na zizi la mbuzi.Katikati ya uwanja kulikuwa na magogo makubwa yakiwaka Moto ambao wenyeji waliutumia kama silaha dhidi ya wanyama wakali vilevile kuchomea vyakula na kujipatia joto msimu wa baridi.
"Shkamoo Mzee, habari za hapa?"Dereva alianza kusalimia pindi tu walipowasili kwenye Moto.
"Salama kijana, Karibuni viazi"Aliitikia Mzee ambae kwa haraka haraka anaweza kuwa na umri wa miaka 70 Kama sio 75.Mzee huyo aliendelea kuongea"kalete viti" Alimwagiza kijana mmoja aliyekuwepo pale.
"Asante sana Mzee"Dereva Aliitikia huku akichukua viazi vitatu vilivyochomwa na kuwakabidhi wenzake,wakati huohuo viti vya asili vilivyotengenezwa kwa fito na ngozi ya mbuzi vililetwa wakaketi.
"Habari za huko mtokako"Aliongea Mzee kwa uchangamfu huku Mara kadhaa akitupia jicho kwa yule binti.
"Salama kiasi Mzee,sisi sio wakaaji Sana tumeharibikiwa usafiri tunaomba msaada wa maji"Aliongea Dereva akatulia kusubiri jibu.
Mzee anamtizama Tena Binti Kama mtu anayekagua vitu kisha anazama kwenye lindi zito la Mawazo kabla hajashtushwa na sauti ya mjukuu wake"Babu wanaomba maji"
"Aaaha maji,maji eeh kwa kweli ndani Sina maji na hapa tunaishi wawili tu,hakuna mwanamke wa kutuchotea maji ila mnaweza kufuata hapo nyuma kidogo Kuna kisima,wee hebu wapeleke kisimani"Kijana anasimama na kuanza kuwaongoza kisimani huku akiwasaidia kubeba dumu.
"Binti wee Baki tu hapa uwasubiri, chukua viazi,kula na karanga"Mzee Aliongea huku akimzuia binti asiende,akamsogezea viazi na karanga,huku akijichekesha chekesha.Baada ya vijana kuelekea kisimani Mzee anaanza vituko,vituko ambavyo havikumfurahisha binti hata kidogo.
"Unaijua hii?,Tamu kuliko asali nikuonjeshe?"Mzee Aliongea huku akishika sehemu zake nyeti akimuonyesha binti, Binti alitetemeka kwa hofu kubwa akaanza kunyanyuka kitini Lakini Mzee alimuwahi akamshika mkono kwa nguvu.Binti aliona hatari ipo mbele yake akaachia ukelele"Mamaaaa"
"shhhhhh kimya takuchinja"Mzee alimpa ishara akae kimya,akachomoa kisu kiunoni mwake na kumuonyeshea jambo lililomtisha zaidi binti akabaki akilia machozi tu pasi na kutoa sauti.
Mzee akapata nafasi ya kukimbia nae akimvutia pembeni kidogo ya nyumba kulikokuwa na kichaka kilichojaa majani na kufanya umbo la duara.Haraka haraka Mzee akaingia na Binti kichakani humo,akamlaza chali mikono yake yenye nguvu ilimdhibiti binti haswa,hakuweza hata kufurukuta alilia kilio Cha samaki machozi baharini,Mzee alikuwa na uchu kupita kiasi ni takribani miaka 3 tangu afiwe na mkewe hakuwahi kupata mwanamke wa kukidhi haja zake za mwili,na sasa alitaka kutuliza tamaa zake, hakujali Kama yule Binti ni mdogo,hakuwa na huruma hata chembe,aliivuta gauni juu ikamfunika binti usoni,chini akakutana na kaptula zito alilovaa binti Kama nguo ya ndani, kaptula lilibana sawasawa kiunoni mwa binti,Mzee akapata kibarua Cha kuanza kuivuta kaptula hiyo huku akitetemeka kwa tamaa zilizopita kiasi.
Je Mzee atafanikiwa kufanya ujinga aliodhamiria?,usichoke kufuatilia simulizi hi,ITAENDELEA...

Post a Comment